Sunday 8 November 2015

Ajali zapokonya maisha wanajamii wakichuma riziki Keumbu, Kisii





Katika bahari ya maisha, kila siku gharama ya maisha inavyozidi kupanda na maisha kuwa magumu, ndivyo wakenya wanavyozidi kukaza kamba katika hatakati ya kutafuta riziki.
Na kwa sababu hii, wananchi katika sehemu ya Keumbu kaunti ya Kisii, wamekuwa wakijihusisha kufanya biashara katika mazingira magumu ambayo wakati mwingine wameshuhudia wenzao wakiaga katika hali ta kuchuma riziki.
Kama anavyotuarifu mwanahabari wetu Franklin Momanyi, kina mama, wana kwa wakubwa huwa wanang'ang'ania mteja wateja katika soko hilo lililo katika barabara kuu ya Kisii Nairobi, huku ikiwawezesha kupata mkate wa kila siku

Ziara ya Papa Francis : Kanisa lachangisha shilingi milioni 124 za maand...



Huku zikiwa zimasalia siku 17 kabla ya Papa Francis kutua humu nchini, shamrashamra za maandalizi zinaendelea kwa kasi, huku kila mdau akijaribu kuhakikisha kuwa mambo yanaenda kama ilivyo pangwa.
Katika kanisa la mtakatifu Paulo Nairobi, waimabaji wanaendelea kupiga msasa, na tumbuizo watakazotumia katika makaribisho ya Papa Nairobi.


Kama mwanahabari wetu Franklin Momanyi anavyotuarifu, haya yanajiri siku moja tu baada ya kuchangishwa shilingi milioni 124.5 katika hafla iliyoongozwa na rais mstaafu Mwai Kibaki, zitakazotumika katika ziara ya Papa humu nchini.

Monday 2 November 2015

Gavana Munya adai wahuni wachochewa na viongozi Meru na Isiolo


Gavana wa Meru Peter Munya ametoa wito kwa serikali kuu kuimarisha  usalama kwa wanachi wa sehemu ya mpaka wa kaunti za  Meru na Isiolo, kufuatia eneo hilo kushuhudia mashambulizi ya mara kwa mara hivi majuzi .

Gavana Munya amesema maswala ya usalama hayajagatuliwa katika katiba  na ni jukumu la serikali kudhibiti hali hiyo kabla haijasambaratika hata zaidi kwani hadi kufikia sasa idadi maasifa wa polisi  katika eneo hilo ni ya chini mno ikilinganishwa na wahalifu wanaoendelea kutekeleza mashambulizi katika eneo hilo

Friday 30 October 2015

KDF washambulia na kuuwa wanamgambo 15 wa Al-shabaab





Kikosi cha wanajeshi wa Kenya chini ya muungano wa Amisom, mapema siku ya Jumapili wamewaangamiza wanamgambo 15 wa Alshabab waliokuwa wakivuka mto Jubba katika eneo la Yantoony kutoka Jilib na kuingia eneo la Juba kusini nchini Somalia.
Kulingana na msemaji wa jeshi la Kenya kanali David Obonyo, shambulizi hilo ni kati ya misururu ya mashambulizi yanayoendelea katika ukanda wa Jubba ili kufanikisha kutwaa eneo la Jilib ambalo ndilo ngome la pekee ya wananamgambo hao kusini mwa Shabelle

Saturday 24 October 2015

MOMBASA DISSAPEARANCE MAN

MRADI WA KWANZA WA AINA YAKE WA KUPEANA MAKAAZI YA KISASA

WAUZAJI POMBE HATARI WAVUMBUA MBINU MPYA ZA KUTEKELEZA BIASHA ZAO




BAADA YA MSIMAMO MKALI KUHUSIANA NA BIASHARA YA POMBE HARAMU NCHINI, SASA WAUZAJI WA POMBE HIYO  KATIKA SOKO LA ELDORET KAUNTI YA UASINGISHU, WALIAMUA KUVUMBUA MBINU YA KUWAWEZESHA KUENDESHA BILA KUJULIKANA NA VYOMBO VYA USALAMA KWA MUDA SASA. 

LAKINI LEO SIKU YA ILIKUWA SIKU YA AROBANNE KWA BAADHI YAO BAADA YA WAUZAJI KUMI IKIWEMO BINTI WENYE UMRI MDOGO, KUNASWA WAKIWA KATIKA HARAKATI YA KUWASHUGHULIKIA WATEJA WAO MJINI ELDORET. 

KAMA MWADISHI WETU FRANKLN MOMANYI ANAVYOTUARIFU, WAUZAJI HAO WAMEAMUA KUWEKA HIRIZI KWENYE  MILANGO YAO ILI KUWAOGOFYA ASKARI WATAKAOENDA KUWAKAMATA

Friday 23 October 2015

Familia haijui binti yao yuhai au amekufa mwaka mmoja tangu aliposafiri





Familia moja katika kijiji cha ngamba eneo bunge la Mathioya sasa imekumbumwa na wingu la taharuki baada ya kukosa kujua aliko mwanao ambaye alikuwa akifanya kazi nchini Saudia Arabia.Mary Muringi ambaye kwa sasa amekuwa mfanyakazi wa nyumba nchini Saudi kwa mwaka muda mmoja, alipigia mamake simu na kumtaka kumwombea baada ya kuzuka mtafaruku baina yake na mwajiri wake.
Kuanzia siku hiyo hawajasemezana tena na wala hapatikani kwa simu.

Senata Kiraitu asema angali anafikiria uwezekano wa kusaka ugavana





Seneta wa Meru Kiraitu Murungi ambaye ni kiongozi wa chama cha APK amesema bado angali anafikiria kuhusu iwapo atawainia kiti cha gavana wa kaunti ya Meru katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2017.
Hii ni kufuatia shinikizo anazopata kutoka kwa viongozi wa sehemu hiyo za kumtaka kumenyana na gavana Peter Munya ambaye kwa sasa, viongozi hao wanasema hawajaridhika na uongozi wake.
Kama anavyotuarifu Franklin Momanyi Munya kwa upande wake anashikilia yuko ngangari kupambana na yeyote yule.

Sunday 18 October 2015

Wazee kutoka Nyeri wafanya tambiko kwa mti kuanguka juma lililopita





Hali ya taharuki imekumba kijiji cha Ngunguru eneo bunge la Mathira kaunti ya Nyeri baada ya mti wa Mugumu, unaokadiriwa kuwa na zaidi ya miaka mia moja kuaguka.
Tukio hili linajiri chini ya saa 48, tangu wazee kutoka jamii hiyo kuzuru eneo la Gamerock kule Nyeri kufanya tambiko kwa ajili ya mti kama huo ulioanguka eneo hilo wiki jana.

Familia haijui binti yao yuhai au amekufa mwaka mmoja tangu aliposafiri



Familia moja katika kijiji cha ngamba eneo bunge la Mathioya sasa imekumbumwa na wingu la taharuki baada ya kukosa kujua aliko mwanao ambaye alikuwa akifanya kazi nchini Saudia Arabia.Mary Muringi ambaye kwa sasa amekuwa mfanyakazi wa nyumba nchini Saudi kwa mwaka muda mmoja, alipigia mamake simu na kumtaka kumwombea baada ya kuzuka mtafaruku baina yake na mwajiri wake.
Kuanzia siku hiyo hawajasemezana tena na wala hapatikani kwa simu.

Saturday 3 October 2015

Meneja wa mikopo Equity auawa, siku moja baada ya zaidi ya sh. milioni 2...





Afisa mmoja anayesimamia mikopo katika makao makuu ya benki ya Equity aliyetekwa nyara na majambazi siku ya Ijumaa usiku, amepatikana amefariki leo asubuhi na mwili wake kuachwa ndani ya
gari lake katika eneo la Redhill huko Limuru.
Kisa hiki kinajiri siku moja tu baada ya wezi waliojidai kuwa wakaguzi
wa vitabu vya hesabu kuzuru benki ya Equity tawi la Othaya jana asubuhi na kuiba zaidi ya shilingi milioni 20.

KUTOKA BAWABU HADI KUMILIKI KAMPUNI!

Sunday 27 September 2015

Waumini wazozana kuhusu madai ya ushoga katika kanisa la ACK Nyeri





Hali ya utata inazidi kukumba kanisa la ACK Kagongo katika parokia ya Othaya, kaunti ya Nyeri, baada ya waumini wa kanisa hilo kuandaa misa mbili sambamba wakati mmoja, hii leo katika majengo ya kanisa hilo.
Kundi moja la waumini hao linalomuunga mkono kiongozi wa kanisa hilo, aliyetimuliwa wiki jana pamoja na wengine wanne, kwa madai ya kuhusika katika masuala ya ushoga, lililazimika kujitenga na wenzao waliondaa misa yao ndani ya kanisa hilo.

Wednesday 9 September 2015

OPERESHENI YA KUWAFURUSHA WANAMGAMBO WA ALSHABAAB





ZAIDI YA FAMILIA  ELFU MOJA ZIMETOA WITO KWA SERIKALI KUTOWAHAMISHA

KUTOKA KWENYE MAKAAZI YAO YA MUDA MREFU NDANI YA MSITU WA BONI, KATIKA

ENEO LA PANDANGUO KWA KISINGIZIO CHA KUWAFURUSHA WANAMGAMBO WA AL

SHABAAB.



BADALA YAKE WAMEIOMBA SERIKALI KUIMARISHA USALAMA KATIKA ENEO HILO NA

KUHAKIKISHA KUWA CHAKULA KIMEWAFIKIA KWANI NJIA ZA KUJIKIMU

ZIMESAMBARATIKA.




Sunday 6 September 2015

Tume ya kuajiri Walimu yaonya kuwafuta wasiporudi kazini jumatatu



Kufuatia uamuzi uliotolea na mahakamani mnamo tarehe 4 mwezi huu kuhusu
mgomo wa walimu, mwajiri wa waalimu TSC amejitokeza kufafanua uamuzi
huo. Alisema kuwa kulingana naye mgomo huo si halali.
Tume hiyo sasa inawataka walimu wote warudi shuleni kufikia siku ya Jumatatu tarehe saba saa mbili asubuhi.
Aidha tume hiyo iliongezea kuwa wale watakaopuuza agizo hilo basi, hawana budi kutimuliwa kutoka kwa orodha ya waalimu chini.

Sunday 30 August 2015

Rais Kenyatta anunua ngombe kwa sh. 900,000 maonyeshoni Mombasa





Ukistaajabu ya musa, jipange kuona ya firauni! Hii ni baada ya waliodhuria maonyesho ya kilimo mjini Mombasa kubaki vinywa wazi baada ya fahali mmoja kumgharimu rais Uhuru Kenyatta shilingi laki tisa ili kummiliki.
Fahali huyo kutoka ADC Galana ranch, amekabidiwa vijana wa hutuma kwa taifa NYS baada ya rais kumnunua kupitia mnada .

Sunday 23 August 2015

KILIFI ALSHABBAB SPOUSES

BEYOND ZERO CAMPAIGN IN WEST POKOT

MOLO EAC RETIREES BENEFITS

KAKAMEGA GOLDMINE COLLAPSE

KISII DEMO OVER DUMPSITE

WOMEN AGAINIST DRUNKARDS

SIX CHIEF SACKED IN EMBU

GEOGRAPHICAL MAPPING USING NEW TCHNOLOGY

MPEKETONI DEMO

TURKANA WATER SHORTAGE

ISIOLO DAY OF THE AFRICAN CHILD

Tuesday 18 August 2015

JE UMEWAI KUONA MTU AMBAYE MIDOMO YAKE IMEFURUKUTIKA? WAKATI AMBAPO
SEHEMU ZOTE MBILI ZA USO; YA KULIA NA KUSHOTO HAZIAMBATANI KWA
KIONYESHA HISIA? BASI UNGOMJWA HUO NI BELL'S PALSY AL MAARUFU BELL"S PALSY

Ferdinand Waititu Aongoza Wananchi Kuvamia Vilabu Huko Wangige





Hali ya taharuki kutanda katika eneo la Wangige kaunti ya Kiambu, wakati wananchi wa sehemu hiyo walipoamua kuvamia vilabu mbali mbali katika juhudi za kukabiliana na pombe haramu.
Wakiongozwa na mbunge wao Ferdnand Waititu, wenyeji hao walivunja chupa na kumwaga pombe hiyo ambayo walisema imewaathiri vijana katika sehemu hiyo.

Diwani wa zamani adaiwa kuwalawiti wanawe 7,Ruiru





Hali ya mshangao imeghubika kijiji kimoja cha Ruiru baada ya kuibuka madai kuwa mwanaume mmoja mwenye umri wa makamo amekuwa akiwalawiti na kuwabaka wanawe saba kwa muda wa miaka miwili sasa.
Duru za kuaminika zasema kuwa kiongozi huyo wa zamani wa wadi ya Ruiru, amekuwa akiwatendea watoto wake wenye umri wa kati ya miaka miwili na kumi na mitano mtawalia, vitendo vya unyama bila ya mama yao kuwa na habari.

Washukiwa waliokuwa wakielekea Somalia wanaswa Garissa





Watu wawili akiwemo mwanamke mkenya walionaswa na polisi wa kitengo cha kukabiliana na ugaidi, wakiwa safarini kuelekea Somalia,siku ya Ijumaa walifikishwa mahakamani mjini Gararisa.
Inadaiwa mwanamke huyo alidhamiria kuolewa na mwanamgambo wa Al shabaab.

Mlemavu aliyetelekezwa na jamaa zake aamua kuishi mwituni, Meru





Mzee mmoja mwenye umri wa miaka sabini alieamua kutengeneza maskani yake ndani ya msitu, baada ya jamaa zake kumtelekeza katika eneo bunge la Maara, kaunti ya Tharaka Nithi. Mzee huyo licha ya ulemavu wake, amedhihirisha ukakamavu wake katika maisha, kwa kuwa na uwezo wa kutoa ushauri nasaha kwa vijana na hata wazee katika jamii hiyo mwanahabari wetu Franklin Momanyi alimtembelea na kutuandalia taarifa ifuatayo.

Mambo unayofaa kuzingatia unapoogelea baharini, ziwani au mtoni



Ni msimu wa likizo wakati ambapo watu wengi hupendelea kutafuta mahali pa kujivinjari na kuondoa msongo wa panda shuka za maisha.
Wana kwa watu wazima aghalabu huelekea Pwani angalau kuogelea na kubarizi kwenye mchanga wa baharini.
Lakini la kutamausha ni kwamba wapo wengi ambao wamekumbwa na majanga makubwa katika harakati hizo kwa mfano, visa vya hivi punde vya kufa maji kwa wanafunzi saba baharini na kuzama kwa wavuvi watatu katika ziwa Naivasha.
Franklin Momanyi anaangazia tahadhari zinazofaa kuchukulia kabla ya kuanza mtu kujitosa majini kuogelea.

Friday 6 March 2015

Matatizo yanayokumba Kiswahili katika sajili ya mauzo/ biashara



Siku hizi za sasa, ni vigumu kuskiza redio bila kuyaskia matangazo ya  kibiashara. Unaposafiri njiani utakumbana na mabango makubwa makubwa yanayopasha wapita njia ujumbe fulani kuhusiana na bidhaa fulani. Kila kitu tunachotangamana nacho kwa njia moja au nyiingine, bila shaka huwa tunakumbana na matangazo ya kibiashara. Hata wakati mwingine tunapokea arafa za kutujulisha kuhusu bidhaa Fulani ama kutupa maelezo ya kutumia bidhaa Fulani. Lakini swali ni je, Kwa hizi njia zote ambazo zimetumika  ili kuwasilisha ujumbe, je lugha ya Kiswahili imetumiwa vipi katika nyanja hiyo? Je kwa njia yeyote ile, Kiswahili kimekuzwa? Na kama kimekuzwa ni kwa nini? Kama kimelemazwa, mbona, na nini kinachangia haswa hali hii?

Kabla ya kuenda mbali sana na makala haya, hebu tugusie  sajili ya biashara kwa sababu matangazo yote ya mauzo au kibiashara yapo katika sajili ya biashara.
·         Hutumia lugha ya chuku sana
·         Msamiati maalum
·         Kuchanganya ndimi
·         Matumizi ya picha na michoro
·         Matumizi ya nyimbo
·         Sentensi ndefundefu pale mteja anapoelezea mteja

Sifa za lugha inayostahili kutumika katika matangazo.
·          Nyepesi
·         Inayoweza fikisha ujumbe kwa mlengwa bila kujikanganya
·         Muktadha unaoeleweka (Context)
·         Inatumia jazanda  (Alex Grijelmo) anasema katika kitabu chake cha  "Seduction of the Words", kuwa matangazo ya mauzo yanatumia jazanda  - huru kama jua "Free as the Sun")
Kulingana na takwimu wakenya wengi  husoma kiingereza kuliko wale wanaopenda kusoma Kiswahili. Haswa hii ndiyo sababu moja ya matangazo mengi ya kibiashara kuwa yameandikwa kwa lugha ya kiingereza. Yakiandikwa kwa kiingereza ndio wanatafsiri ili kuwafikia wapenzi wa Kiswahili. Mara nyingi wakifanya utafsiri, kuna uwezo wa wao kupotoka na kutumia lugha ambayo si sanifu. Kwa mfano, Lipo tangazo linalosema ‘Triatix is for both small scale farmers and large scale farmers” linapotafsiriwa kuwa; Triatix ni ya wakulima  wadogowadogo na wakulima  wakubwa badala ya kusema, wakulima wenye mashamba madogomadogo na wale wenye mashamba makubwa makubwa.

Kiswahili kinanyanyaswa na kulemazwa sana na mahoka ambao mara nyingi hufikiria kwamba,  ili kuchekesha wakenya, lazima uvunje kaida za Kiswahili. Kwa mfano utasikia mahoka akiwa ulingoni akisema “Mtoto chake…..” Hii ni sawa?  Lakini tukumbuke kuwa wakenya wengi ndio wamesaidia kujenga hii taswira katika fikra zao. Naomba siku moja wakenya wagutuke na kuanza kuwa polisi wa lugha ya Kiswahili. Wakiona mtu akivunja sheria za kisarufi  basi moja kwa moja wamkosoe.

Tatizo lingine ambalo naweza sema kuwa linaleta shida ni watu kuwa na uzembe wa kutonunua kamusi ya kibiashara  na unchumi (TUKI) sababu ipo madukani. Na wakati mwingiine tukinunua, hatupati wakati wa kuiangalia. Kwa mfano matangazo mengi ya kibiashara huwa yanatumia neno “interest” badala ya riba, ama katika tangazo lile la Sona moja; kijana wa kimasai anasema “kichwa anauma” hii ni kuvunja sheria za kisarufi  kwa sababu kichwa kipo katika ngeli na KI-VI. Nashangaa angesema kichwa kinauma, ina maana hangeeleweka? Na watu wakiskia ile taasis wanayoiezi ikitumia jina la kiingereza kwa Kiswahili  ama kuvunja ngeli basi bila shaka nao hawatasita kufanya  vivyo hivyo. Na kwa kweli huwa hali hii inalemaza Kiswahili.

Changamoto nyingine ni kwamba baadhi ya misamiati inayotumika katika katika  mauzo haswa ya kitechnolojia haijapata kupatikana kwa Kiswahili. Kwa mfano; lile tangazo la faiba; “8bits per second” kwa kweli huwa ni vigumu kupata misamiati ya Kiswahili kuashiria hilo.

Wakati mwingine ni ukosefu wa uzoefu wa kutumia misamiati Fulani katika lugha ya mauzo. Lengo kuu la lugha ya mauzo ni kuhakikisha kwamba msikilizaji wa ujumbe ule ameweza kukunua bidhaa ama huduma inayotangazwa. Kwa sababu hii inawabidi kutumia lugha ambayo inaeleweka haraka na walengwa wa ujumbe ule. Kwa mfano; karo,kodi,rubuni, riba, kiinuamgongo ni aina ya malipo

Kulingana na takwimu, kuhesabu idadi ya watu nchini Kenya (2009),  wakenya wengi huskiliza Kiswahili mara nyingi   kuliko wale wanao skiliza redio za lugha ya kiingereza. Hii ina maana kwamba watu wengi huzungumza Kiswahili kwa sababu ki karibu na lugha zao za mama ambazo kwa aina Fulani zinakaribiana na kibantu. Swala hili linafanya redio zinazopererusha matangazo kwa lugha za Kiswahili kutangulia kwa idadi ya waskilizaji nchini. Kwa mfano, Citizen yaongozwa ikifwatiwa na radio jambo kisha redio maisha. Kisha stesheni  hizo zinapata mapato makubwa kutokana na mauzo ya jumbe za kibiashara. Kutokana na hii sababu, wanabiashara hujaribu kutumia Kiswahili ili kuwafikia wakenya wengi ambao huelewa Kiswahili kwa urahisi kuliko kiingereza ili kuongeza mauzo
mbalimbali.

Baadhi ya changamoto zinazokumba matumizi ya Kiswahili katika lugha ya mauzo/kibiashara.
1.       Ukosefu wa istlahi zilizo sawazishwa na kusanifishwa kutumika katika sajili ya biashara.
Kwa mfano
2.       Ukosefu wa uzoefu wa  kutumia kamusi za kibiashara (TUKI) kubaini maneno sahihi ya kutumia katika mustakabali mbalimbali.
3.       Ukosefu wa wa chombo maalum cha kuratibu shughuli nzima ya ukusanyanyaji, usanifishaji na hata usambazaji wa istalahi mpya za kibiashara katika vyombo vyote vya habari nchini
4.       Kwa sababu ya kutaka kueleweka kwa urahisi, wanabiashara hutumia lugha zingine mfano wa lugha ibuka kama SHENG ili kueleweka na hadhira ama walengwa wa ujumbe. Kwa mfano “shinda hao” na KCB
5.       Wale ambao wametwikwa jukumu la kutafsiri matangazo ya Kiswahili hawaelewi fika sheria, kaida na miiko inayoandamana na utumizi wa lugha ya Kiswahili.
6.       Ukosefu wa visawe au maneno yaliyo na maana sawa katika lugha asilia  na lugha pokezi kwa mfano bidhaa zinazohusiana na maswala ya kiteknolojia kama vile data bundles kwa matangazo ya bidhaa za mawasiliano.

Lakini si wakati wote ambapo Kiswahili kimelemazwa. Wapo wengine ambao ambao hukuza Lugha ya Kiswahili kwa mfano wale wanaoleta tangazo la sabuni ya ariel ambaopo wanasema madoa sugu badala ya madoadoa kama wengine husema.

Suluhisho la pekee kwa suala hili ni kurekebisha makosa hayo tumeangalia hapo awali ili tuweze kuwa na nafasi muhimu ya kuinua nafasi muhimu ya kukikuza Kiswahili chetu.
Kwa mfano; tubadilishe hii kasumba ya mahoka kuwa wakivunja kanuni za Kiswahili tusicheke,  na hilo litawabidi wabadirishe mbinu. itakuwa bora kusikia wa kenya wameanza kukitukuza Kiswahili na hili litawafanya wale wanaotunga jumbe za mauzo au  kibiashara kuzingatia sheria.
Pili wawe wakiajiri watu waliosomea taaluma  ya utafsiri kwa sababu makosa mengi tunayoyaona ni ni ya kutafsiri. Na kwa jumla kurekebisha Masuala ambayo tumeshayaguzia hapo awali…

Mtayarishi:  Frankline Momanyi
Chuo Kikuu cha Chuka.