Siku hizi za sasa, ni vigumu kuskiza redio bila kuyaskia
matangazo ya kibiashara. Unaposafiri
njiani utakumbana na mabango makubwa makubwa yanayopasha wapita njia ujumbe
fulani kuhusiana na bidhaa fulani. Kila kitu tunachotangamana nacho kwa njia
moja au nyiingine, bila shaka huwa tunakumbana na matangazo ya kibiashara. Hata
wakati mwingine tunapokea arafa za kutujulisha kuhusu bidhaa Fulani ama kutupa
maelezo ya kutumia bidhaa Fulani. Lakini swali ni je, Kwa hizi njia zote ambazo
zimetumika ili kuwasilisha ujumbe, je
lugha ya Kiswahili imetumiwa vipi katika nyanja hiyo? Je kwa njia yeyote ile,
Kiswahili kimekuzwa? Na kama kimekuzwa ni kwa nini? Kama kimelemazwa, mbona, na
nini kinachangia haswa hali hii?
Kabla ya kuenda mbali sana na makala haya, hebu tugusie sajili ya biashara kwa sababu matangazo yote
ya mauzo au kibiashara yapo katika sajili ya biashara.
·
Hutumia lugha ya chuku sana
·
Msamiati maalum
·
Kuchanganya ndimi
·
Matumizi ya picha na michoro
·
Matumizi ya nyimbo
·
Sentensi ndefundefu pale mteja anapoelezea mteja
Sifa za lugha inayostahili kutumika katika matangazo.
·
Nyepesi
·
Inayoweza fikisha ujumbe kwa mlengwa bila
kujikanganya
·
Muktadha unaoeleweka (Context)
·
Inatumia jazanda (Alex Grijelmo) anasema katika kitabu chake
cha "Seduction of the Words", kuwa matangazo ya mauzo yanatumia
jazanda - huru kama jua "Free as
the Sun")
Kulingana na takwimu wakenya wengi husoma kiingereza kuliko wale wanaopenda
kusoma Kiswahili. Haswa hii ndiyo sababu moja ya matangazo mengi ya kibiashara
kuwa yameandikwa kwa lugha ya kiingereza. Yakiandikwa kwa kiingereza ndio
wanatafsiri ili kuwafikia wapenzi wa Kiswahili. Mara nyingi wakifanya utafsiri,
kuna uwezo wa wao kupotoka na kutumia lugha ambayo si sanifu. Kwa mfano, Lipo
tangazo linalosema ‘Triatix is for both
small scale farmers and large scale farmers” linapotafsiriwa kuwa; Triatix
ni ya wakulima wadogowadogo na
wakulima wakubwa badala ya kusema, wakulima
wenye mashamba madogomadogo na wale wenye mashamba makubwa makubwa.
Kiswahili kinanyanyaswa na kulemazwa sana na mahoka ambao
mara nyingi hufikiria kwamba, ili
kuchekesha wakenya, lazima uvunje kaida za Kiswahili. Kwa mfano utasikia mahoka
akiwa ulingoni akisema “Mtoto chake…..” Hii
ni sawa? Lakini tukumbuke kuwa wakenya
wengi ndio wamesaidia kujenga hii taswira katika fikra zao. Naomba siku moja
wakenya wagutuke na kuanza kuwa polisi wa lugha ya Kiswahili. Wakiona mtu akivunja
sheria za kisarufi basi moja kwa moja
wamkosoe.
Tatizo lingine ambalo naweza sema kuwa linaleta shida ni
watu kuwa na uzembe wa kutonunua kamusi ya kibiashara na unchumi (TUKI) sababu ipo madukani. Na
wakati mwingiine tukinunua, hatupati wakati wa kuiangalia. Kwa mfano matangazo
mengi ya kibiashara huwa yanatumia neno “interest” badala ya riba, ama katika
tangazo lile la Sona moja; kijana wa kimasai anasema “kichwa anauma” hii ni kuvunja sheria za kisarufi kwa sababu kichwa kipo katika ngeli na KI-VI.
Nashangaa angesema kichwa kinauma, ina maana hangeeleweka? Na watu wakiskia ile
taasis wanayoiezi ikitumia jina la kiingereza kwa Kiswahili ama kuvunja ngeli basi bila shaka nao
hawatasita kufanya vivyo hivyo. Na kwa
kweli huwa hali hii inalemaza Kiswahili.
Changamoto nyingine ni kwamba baadhi ya misamiati
inayotumika katika katika mauzo haswa ya
kitechnolojia haijapata kupatikana kwa Kiswahili. Kwa mfano; lile tangazo la
faiba; “8bits per second” kwa kweli huwa ni vigumu kupata misamiati ya
Kiswahili kuashiria hilo.
Wakati mwingine ni ukosefu wa uzoefu wa kutumia misamiati
Fulani katika lugha ya mauzo. Lengo kuu la lugha ya mauzo ni kuhakikisha kwamba
msikilizaji wa ujumbe ule ameweza kukunua bidhaa ama huduma inayotangazwa. Kwa
sababu hii inawabidi kutumia lugha ambayo inaeleweka haraka na walengwa wa
ujumbe ule. Kwa mfano; karo,kodi,rubuni, riba, kiinuamgongo ni aina ya malipo
Kulingana na takwimu, kuhesabu idadi ya watu nchini Kenya (2009), wakenya wengi huskiliza Kiswahili mara nyingi
kuliko wale wanao skiliza redio za lugha ya
kiingereza. Hii ina maana kwamba watu wengi huzungumza Kiswahili kwa sababu ki
karibu na lugha zao za mama ambazo kwa aina Fulani zinakaribiana na kibantu.
Swala hili linafanya redio zinazopererusha matangazo kwa lugha za Kiswahili
kutangulia kwa idadi ya waskilizaji nchini. Kwa mfano, Citizen yaongozwa
ikifwatiwa na radio jambo kisha redio maisha. Kisha stesheni hizo zinapata mapato makubwa kutokana na mauzo
ya jumbe za kibiashara. Kutokana na hii sababu, wanabiashara hujaribu kutumia
Kiswahili ili kuwafikia wakenya wengi ambao huelewa Kiswahili kwa urahisi kuliko
kiingereza ili kuongeza mauzo
mbalimbali.
Baadhi ya changamoto zinazokumba
matumizi ya Kiswahili katika lugha ya mauzo/kibiashara.
1.
Ukosefu wa istlahi zilizo sawazishwa na kusanifishwa
kutumika katika sajili ya biashara.
Kwa mfano
2.
Ukosefu wa uzoefu wa kutumia kamusi za kibiashara (TUKI) kubaini
maneno sahihi ya kutumia katika mustakabali mbalimbali.
3.
Ukosefu wa wa chombo maalum cha kuratibu
shughuli nzima ya ukusanyanyaji, usanifishaji na hata usambazaji wa istalahi
mpya za kibiashara katika vyombo vyote vya habari nchini
4.
Kwa sababu ya kutaka kueleweka kwa urahisi,
wanabiashara hutumia lugha zingine mfano wa lugha ibuka kama SHENG ili
kueleweka na hadhira ama walengwa wa ujumbe. Kwa mfano “shinda hao” na KCB
5.
Wale ambao wametwikwa jukumu la kutafsiri
matangazo ya Kiswahili hawaelewi fika sheria, kaida na miiko inayoandamana na
utumizi wa lugha ya Kiswahili.
6.
Ukosefu wa visawe au maneno yaliyo na maana sawa
katika lugha asilia na lugha pokezi kwa
mfano bidhaa zinazohusiana na maswala ya kiteknolojia kama vile data bundles kwa matangazo ya bidhaa za
mawasiliano.
Lakini si wakati wote ambapo Kiswahili kimelemazwa. Wapo
wengine ambao ambao hukuza Lugha ya Kiswahili kwa mfano wale wanaoleta tangazo
la sabuni ya ariel
ambaopo wanasema madoa sugu badala ya madoadoa kama wengine husema.
Suluhisho la pekee kwa suala hili ni kurekebisha makosa hayo
tumeangalia hapo awali ili tuweze kuwa na nafasi muhimu ya kuinua nafasi muhimu
ya kukikuza Kiswahili chetu.
Kwa mfano; tubadilishe hii kasumba ya mahoka kuwa wakivunja
kanuni za Kiswahili tusicheke, na hilo
litawabidi wabadirishe mbinu. itakuwa bora kusikia wa kenya wameanza kukitukuza
Kiswahili na hili litawafanya wale wanaotunga jumbe za mauzo au kibiashara kuzingatia sheria.
Pili wawe wakiajiri watu waliosomea taaluma ya utafsiri kwa sababu makosa mengi
tunayoyaona ni ni ya kutafsiri. Na kwa jumla kurekebisha Masuala ambayo tumeshayaguzia
hapo awali…
Mtayarishi: Frankline Momanyi
Chuo Kikuu cha Chuka.
No comments:
Post a Comment