Thursday 30 October 2014

Wazazi wapata afueni


Wanafunzi wa shule ya uoili wakiwa kwenye mahabara.

Mapendekezo yaliyotolewa na jopo la kutathmini karo za shule za upili ni mwafaka iwapo yataidhinishwa. Mapendekezo hayo ya kupunguza karo kwa wanafunzi wa shule za upili za umma yanafaa na ni afueni kwa wazazi ambao kidogo wamekuwa wakitwika mzigo mkubwa sana wa kulipa kitita kikubwa cha fedha kila mwaka.

Tume hiyo inayoongozwa na aliyekuwa wazili wa elimu Dkt Kilemi Mwiria ambaye sasa ni mshauri wa rais kuhusu maswala ya elimu iliwasilishe ripoti yenye mapendekezo hayo kwa rais ambaye aliyapokea kwa mwelekeo chanya na kusema kuwa kila motto anapaswa kupata elimu ya kimsingi. Aidha rais aliongeza kusema kuwa serikali kuu itashirikiana na idara nyingine pamoja na washikadau husika kuhakikisha kuwa hili litatimia.

Hatua hii itahakikisha kuwa visa vya wanafunzi kuacha shule kwa ajili ya ukosefu wa karo imezimwa hivyo kwa wanafunzi ambao huzembea katika masomo yao na kuacha shule hawatawa na sababu ya kuacha hivyo basi waweza wakachukuliwa hatua za kisheria. Hii pia itatoa nafasi sawa kwa kila mwanafunzi kupata elimu. Ni matumaini ya kila mzazi kuwa Rais ataidhinisha mapendekezo hayo baada ya mashauriano na washikadau wote katika sekta ya elimu.

 Mwandishi ni Mburu Samwel
(Chuo Kikuu cha Chuka.)

Tuesday 28 October 2014

JANGA KUBWA VYUONI



Wanafunzi wengi hupata furaha wanapopata fursa ya kujiunga na chuo kikuu. Kwa  mfano, nilipopata barua yangu mwaka wa pili baada ya kuhitimu masomo ya kidato cha nne. Ilikuwa furaha, shangwe, na nderemo kijijini mwetu kwa kuwa mwana wao alikuwa anajiunga na chuo kikuu. Chuoni ni mahali ambapo mja akiingia akitoka atatoka akiwa mtu wa thamani sana katika taifa lake. Ndo maana wote wanafuzu vyuoni huwa  nguvu kazi ya taifa na wanatumiwa kuendeleza uchumi wa dola. Lakini sasa, hiyo sifa imeanza kufifia na kudidimia. Kwa nini?

 Kitambo kidogo, wanafunzi waliofuzu kwenda chuo kikuu walikuwa wanakaa nje ya chuo kikuu kwa mwaka mmoja na nusu ivi kabla ya kuingia chuoni.  Lakini kutoka mwaka wa 2011, wakati Naibu wa Rais,  Bw. William Ruto alipokuwa Waziri wa Elimu ya Juu, wanafunzi wamekuwa wakijiunga na vyuo moia kwa moja.

Jambo nzuri lakini kulingana na wakati huu,  naona yapo maafa mengi yanakumba vyuo vikuu. Hawa wanafunzi wanapata shida  ya kudhibiti mhemko na kutoamini kwamba apo vyuoni. Mahali ambapo pana uhuru wasio kadiria. Uhuru mkubwa kiasi kwamba hamna sare za kuvalia, kila mmoja ana hiari ya kuvalia gwanda analoliona lamfaa. Ndiposa sasa tunavyo zungumza, ukipitapita vibarabara vya chuo chochote kile mfano ukiwa chuo cha Chuka, utatamaushwa na mavazi utakayo yaona. Juzi mzazi mmoja alizirai alipomwona mwanaye amevalia jinsi hakuwa ametarajia kawe.

Shida nyingine ni ulevi wa pombe na mihadarati. Kwa miaka nimekwa chuoni mwaka wanne sasa, mwaka huu mambo yamekuwa makali kuliko miaka yaote. Wanafunzi haswa wa kike wanabugia mvinyo hadharani bila kujali yeyote wala kuogopa sheria kali za chuo! Zinawafanya mpaka kupigana kisha kuvunja sheria za chuo. Linalonishangaza ni kwamba hawana habari kwamba hapa hakuna kutumwa mzazi nymbani! Ole wao kwa sababu wengi wako mbioni kuonana na jopo la kushughulika nidhamu. Kwani yeyote ambaye amewahi kufika mbelel yake, adhabu ni kubwa na wengi wao kuivumilia ni shida kwa sababu haistahimiliki maishani mwao. Lakini lisilo budi hubidi na ukiyavulia nguo lazima uyakoge ishara ya kukubali adhabu.

Nimeshuhudia mimi wanafunzi wakipatatna asubuhi mchana wameoana na jioni wanafukuzana kisha kesi naletewa mimi. Ngono kiholelaholela, na kutofwatilia ule mpangilio uliowekwa ili kuendesha maisha chuoni. Hili limekuwa likiwapa tumbo joto viongozi wa wanafunzi vyuoni nikiwa mmoja wao. Haswa idara yangu ikiwa ni ya kushughulikia maslahi ya wanafunzi chuoni.

Badala ya kusoma, wapo mtandaoni wakitumia mtandao kuwasiliana, katika mitandao ya kijamii. Maadam tovuti za ngono zimefungwa, hawangebanduka mle.  Mtihani ukifika, baadhi yao wanandika mpaka ukuta almradi wapite kwa kuwa wakianguka hamna jingine ila kwenda nyumbani. Ndo sababu ya kufanya lolote kuokoa maisha yake chuoni.

Nimeona uongozi umejaribu kuweka mikakati ya kukabiliana na haya lakini bado maji yamezidi unga. Ninawaona washauri nasaha wakiwa mbioni lakini mbio zao ni za sakafuni ambazo mpaka sasa zinaishia ukingoni. Makundi ya madhehebu mbalimbli mbalimbali chuoni yakijaribu kuleta msaada. Bado sijaoni dalili ya matumaini lakini lipo tumaini.

Kulingana nami, kuwa katika nafasi ya kurudisha hadhi ya chuo kikuu, lazima warudishe ule mfumo wa kitambo. Kuokoa malemgo ya chuo kikuu kisimama imara, sharti serikali irudishe ule mfumo wa kitambo ili hawa wanafunzi wapate kuona maisha kudogo kabla ya kujiunga na chuo kwa sababu hilo litafawafanya kubadili msimamo wao kuhusu maisha na kutia bidii. Na pia kukomaa kidogo.
Pili nimeletewa kesi nyingi sana za wanafunzi ambao hawana pesa za kuwafanya wawe chuoni. Nikiangalia wale wengi wanakuja katika hali ya uchochole kwa sababu ya msingi wa familia labda. Lakini ukiangazia vizuri, huyu mwanafunzi angekubaliwa kukaa nje kwa miaka miwili kama ilivyokuwa zamani, angetengeneza hela kidogo za kumsaidia kusukuma maisha. Akifika chuoni, ni kuamsha balaa na belua. Hata kukidhi mahitaji yake ni shida. Karo nayo ni mlima unaowapa kiwewe kuukwea.

Kwa sasa inabidi  ukumbuke kwamba ile taasisi ya kupoeana mikopo kwa wanafunzi wa vyuo (HELB) pia haina  hela za kutosha kukidhi mahitaji ya wanafunzi wengi wanaongezeka kila kukicha. Pia taasisi hiyo haina lingine ila kutekeleza amri ya selikali ya kusema iwape wanavunzi wa vyu anuai mikopo. Usisahau kwamba taasis hiyo pia ina jukumu la kuwapa mikopo wale wanafunzi wanaosomea ugaibuni. Kinaya ni kwamba bado hawajaongezewa  fedha kutoka hazina kuu ya kitaifa. Ndio maana tutaendelea kuona migomo ya wanafunzi wa vyuo wakilalamikia ukosefu wa pesa.

Fauka ya hayo, mgaala muue na haki mpe. Si wanafunzi wote ni watovu wa nidhamu. Wapo wenye maadili. Ukiwaangalia vizuri unaweza sema wana malezi ya pende mbili. Hao hufanya kile walinachostahili kufanya na hao ndio hutia for a katika Nyanja mbalimbali ya kimasomo na hata spoti. Na hao ndiyo kila mtu na hata selikali inajivunia.
 Ninapokamilisha ni vizuri kuuliza swali? Je ni nani anayestahili kulaumiwa ka kupungua nidhamu  katika vyuo vyetu?
Mwandishi ni Frankline Momanyi, Mwanafunzi  Chuo Kikkuu cha Chuka.

Tangazo....



Iwapo wewe ni mpenzi wa Kiswahili na una uwezo wa kuandika makala kuhusu jambo lolote katika lugha sanifu ya Kiswahili basi unaweza jiunga na waandishi wengine mashuhuri  wanaoandikia  FAHAMONLINE(www.fahamonline.blogspot.com ). Ukiandika makala yako yatume kwa franklinpendo@gmail.com
Fanya hima ili usije ukabaki nyumba.

Friday 24 October 2014

Hongera kiswahili.


Mimi kama kiumbe niliyebahatika kuzaliwa katika sayari hii, nimemeamua kukupa kongole ewe Malkia Kiswahili kwa sababu wewe ni shujaa. Licha ya madhila yote tumewahi kukufanyia sisi kama waja hapa duniani, wewe umekuwa mkarimu kwa kutufanyia fadhila nyingi ambazo sisi binadam hatukustahili machoni pako. Kwa hilo, pokea  shukran sufufu kutoka kwangu kwa niamba ya wapenzi wako wote duniani.

Naomba niguzie zile njia umeonyesha ukakamavu na ushujaa wa hali ya juu kwa kustahimili mawimbi makali na tufani zinazotokea katika bahari hii ya maisha. Wengi wamejaribu kwa udi na uvumba kukunyang`anya kizazi cha bala lako afrika. Mahali ambapo wewe ulizaliwa na ukafaham kuwa nyumbani. Niliona wakikunyanganya hata watoto wadogo kwe  shule ya chekechekea. Niliona wakipokea mijeledi mikali kwa sababu ya kukuhusudu na kukuenzi, lakini ulifika na kuwafariji kwa mishororo ya kuliwaza nyoyo zao zilizo umia. Na kwa wale hawakukufa moyo, nawaona mahali uliwafikisha ewe Kiswahili. 

Wengine wamepokea hadhi kubwa sana duniani. Sina haja ya kuwataja majina kwa sababu unawajua  bayana ila niseme hao ni wanao kindakindaki. Wapo wale wakereketwa wa kukutaftia mahali pako katika jamii. Bila  kumsahau Yule mwanao Usadh Wala bin Wala. Si unajua mpaka ameanzisha Chuo cha Wasta? 
 Chuo ambacho kinaeneza kila mbinu muhimu ya kukupatia wana wengi wa afrika na jirani zake.

Nimeona ukiwashukuru wanao na wapenzi kindakindaki. Mimi kwanza ulifanya nikaja chuo kikuu sasa nami ni mwana mlimani! Wengine umewatunuku nafasi ya kupaa juu angani mpaka ng`ambo ya maji. Wengine uliwapa ajira na ukawapa shukran sufufu kwa kuinua kipato chao.

Hongera kwa kustahimili mawindo ya wale wanao kuwinda ili wakuangamize. Hawa ni wale wanaowadharau wanao wanaokuenzi kindakindaki wakisema wanaozungumza Kiswahili wana hadhi ya chini. Wengine wamo mbioni kueneza kasumba kwamba Kiswahili ni kigumu, Vipi na tangu lini mwana wa mji akaita mgeni Baba? Ama kweli wamewachanganya baadhi ya wanao. Licha ya hayo nimekuona ukiwatuma wajumbe wako kukutetea katika mijadala yetu na hata ya kimataifa. Kwa kweli wewe ni mwerevu hakika.

Nimeona kiamboni wengine wamekuja na lugha zingine ili wakutoe katika ramani ya dunia. Wameleta sheng`  ili wakunyang`anye hadhira kwa wana wa miji na vijiji. Jambo moja limenishangaza, ni jinsi ambavyo wewe unaendelea kusambaa kote duniani. Nimewaona wanao wakipeleka ujumbe wako mbali na nyumbani ugaibuni. Marekani, China, Ulaya wote wako mbioni kusoma sheria na kaida zako ili wawe na nafasi katika karne hii ya utandawazi. Nimekuona umepenya mpaka ndani ya technologia. Nina furaha kwa sababu niliyaona makao yako kwenye mtandao. Bila shaka hutakufa kipenzi changu Kiswahili. Sasa kamusi nyingi nimeziona zinazokuangazia wewe, na hata katika katiba ya Kenya wewe ulijioatia nafasi yako madhubiti katika dola hili.

Afrika yote inakukumbatia tena kwa hamu. Kuna jambo ambalo nimeliona ukilifanya lakini bado halijatimia. Sio lazima niwe nabii lakini ninauwezo wa kusema hivi karibuni utakuwa wa kutumika Afrika nzima. Nimewaona wakitafuta lugha moja ya kuwaunganisha  wana Afrika na alama zako ziko kidedea kuliko lugha za  Fulani, Yoruba, Mande na Hausa ambazo zilipigiwa kura kujitoza ulingoni kukabiliana nawe. Lakini linalo nipa tabasamu, ni kwamba wewe bado uko mbali na wenzio kwa sababu ya historia yako ndefu na machapisho kadha wa kadha. Pili usuli wako ni wa kibantu na lugha nyingi Afrika ni za kibantu na ndio maana ikilinganishwa na wenzako, wewe una wasemaji wengi. Ndio maana wasomi kama Wole Soyinka, Mohammed  Hasan Abdulaziz na wengine walipokutana mjini Lagos Mwaka wa 1976, walikupigia  kura na hakika hiyo siku itafika kipenzi changu na utafikwa koja.

Ombi langu kuu kwako ni kwamba endelea kuzidi kung`ang`ana na hatimaye utafanikiwa. Ndio najua una shida kidogo kidogo kama za misamiati mingi tu ya kueleza mambo mengi ya kisayanzi na kiteknologia lakini usife moyo kwani wenzako pia wamekopa. Hata wewe una uhuru wa kukopa. Licha ya hayo watie wanao shime ili wasichoke katika utafiti kila siku na kuleta misamiati kwa sababu wewe unakua kwa njia moja kubwa sana.

Nakuomba uzidi kuwakumbusha wale wanao eneza dhana potovu kwamba wewe ni wa haiba ya chini ukiwapa mifano ya wanao wengi ambao wameendelea sana kimaisha kupitia kukukumbatia  wewe. Nangoja kuona siku ile utatumika kama nembo ya kutambulisha Afrika na dunia kwa jumla. Hakika hongera kipenzi changu  kwa juhudi kubwa ulizonazo kwa kuwafaidi wanadam na njia mufidi ya kuwasiliana. Mungu azidi kuwabariki wana na wapenzi wako duniani. 

Mwandishi: Franklin Momanyi.  Mwanafunzi Chuo Kikuu cha Chuka. 


Thursday 23 October 2014

Mti unaobubujika maji katika kigogo chake



Mti mmoja katika mkoa wa Hamedan, magharibi mwa Iran umevutia watu wengi baada ya kububujika maji kwa wingi katika kigogo chake.
Wapita njia walivutiwa na mti huo, baadhi wamepiga picha, baadhi yao wamenawa nyuso, baadhi wamekinga maji hayo kwenye mifuko na vigeleni, alimradi umekuwa kivutio kwa watu mbalimbali.




 kwa Hisani ya Iran Swahili Radio.