Tuesday 28 October 2014

JANGA KUBWA VYUONI



Wanafunzi wengi hupata furaha wanapopata fursa ya kujiunga na chuo kikuu. Kwa  mfano, nilipopata barua yangu mwaka wa pili baada ya kuhitimu masomo ya kidato cha nne. Ilikuwa furaha, shangwe, na nderemo kijijini mwetu kwa kuwa mwana wao alikuwa anajiunga na chuo kikuu. Chuoni ni mahali ambapo mja akiingia akitoka atatoka akiwa mtu wa thamani sana katika taifa lake. Ndo maana wote wanafuzu vyuoni huwa  nguvu kazi ya taifa na wanatumiwa kuendeleza uchumi wa dola. Lakini sasa, hiyo sifa imeanza kufifia na kudidimia. Kwa nini?

 Kitambo kidogo, wanafunzi waliofuzu kwenda chuo kikuu walikuwa wanakaa nje ya chuo kikuu kwa mwaka mmoja na nusu ivi kabla ya kuingia chuoni.  Lakini kutoka mwaka wa 2011, wakati Naibu wa Rais,  Bw. William Ruto alipokuwa Waziri wa Elimu ya Juu, wanafunzi wamekuwa wakijiunga na vyuo moia kwa moja.

Jambo nzuri lakini kulingana na wakati huu,  naona yapo maafa mengi yanakumba vyuo vikuu. Hawa wanafunzi wanapata shida  ya kudhibiti mhemko na kutoamini kwamba apo vyuoni. Mahali ambapo pana uhuru wasio kadiria. Uhuru mkubwa kiasi kwamba hamna sare za kuvalia, kila mmoja ana hiari ya kuvalia gwanda analoliona lamfaa. Ndiposa sasa tunavyo zungumza, ukipitapita vibarabara vya chuo chochote kile mfano ukiwa chuo cha Chuka, utatamaushwa na mavazi utakayo yaona. Juzi mzazi mmoja alizirai alipomwona mwanaye amevalia jinsi hakuwa ametarajia kawe.

Shida nyingine ni ulevi wa pombe na mihadarati. Kwa miaka nimekwa chuoni mwaka wanne sasa, mwaka huu mambo yamekuwa makali kuliko miaka yaote. Wanafunzi haswa wa kike wanabugia mvinyo hadharani bila kujali yeyote wala kuogopa sheria kali za chuo! Zinawafanya mpaka kupigana kisha kuvunja sheria za chuo. Linalonishangaza ni kwamba hawana habari kwamba hapa hakuna kutumwa mzazi nymbani! Ole wao kwa sababu wengi wako mbioni kuonana na jopo la kushughulika nidhamu. Kwani yeyote ambaye amewahi kufika mbelel yake, adhabu ni kubwa na wengi wao kuivumilia ni shida kwa sababu haistahimiliki maishani mwao. Lakini lisilo budi hubidi na ukiyavulia nguo lazima uyakoge ishara ya kukubali adhabu.

Nimeshuhudia mimi wanafunzi wakipatatna asubuhi mchana wameoana na jioni wanafukuzana kisha kesi naletewa mimi. Ngono kiholelaholela, na kutofwatilia ule mpangilio uliowekwa ili kuendesha maisha chuoni. Hili limekuwa likiwapa tumbo joto viongozi wa wanafunzi vyuoni nikiwa mmoja wao. Haswa idara yangu ikiwa ni ya kushughulikia maslahi ya wanafunzi chuoni.

Badala ya kusoma, wapo mtandaoni wakitumia mtandao kuwasiliana, katika mitandao ya kijamii. Maadam tovuti za ngono zimefungwa, hawangebanduka mle.  Mtihani ukifika, baadhi yao wanandika mpaka ukuta almradi wapite kwa kuwa wakianguka hamna jingine ila kwenda nyumbani. Ndo sababu ya kufanya lolote kuokoa maisha yake chuoni.

Nimeona uongozi umejaribu kuweka mikakati ya kukabiliana na haya lakini bado maji yamezidi unga. Ninawaona washauri nasaha wakiwa mbioni lakini mbio zao ni za sakafuni ambazo mpaka sasa zinaishia ukingoni. Makundi ya madhehebu mbalimbli mbalimbali chuoni yakijaribu kuleta msaada. Bado sijaoni dalili ya matumaini lakini lipo tumaini.

Kulingana nami, kuwa katika nafasi ya kurudisha hadhi ya chuo kikuu, lazima warudishe ule mfumo wa kitambo. Kuokoa malemgo ya chuo kikuu kisimama imara, sharti serikali irudishe ule mfumo wa kitambo ili hawa wanafunzi wapate kuona maisha kudogo kabla ya kujiunga na chuo kwa sababu hilo litafawafanya kubadili msimamo wao kuhusu maisha na kutia bidii. Na pia kukomaa kidogo.
Pili nimeletewa kesi nyingi sana za wanafunzi ambao hawana pesa za kuwafanya wawe chuoni. Nikiangalia wale wengi wanakuja katika hali ya uchochole kwa sababu ya msingi wa familia labda. Lakini ukiangazia vizuri, huyu mwanafunzi angekubaliwa kukaa nje kwa miaka miwili kama ilivyokuwa zamani, angetengeneza hela kidogo za kumsaidia kusukuma maisha. Akifika chuoni, ni kuamsha balaa na belua. Hata kukidhi mahitaji yake ni shida. Karo nayo ni mlima unaowapa kiwewe kuukwea.

Kwa sasa inabidi  ukumbuke kwamba ile taasisi ya kupoeana mikopo kwa wanafunzi wa vyuo (HELB) pia haina  hela za kutosha kukidhi mahitaji ya wanafunzi wengi wanaongezeka kila kukicha. Pia taasisi hiyo haina lingine ila kutekeleza amri ya selikali ya kusema iwape wanavunzi wa vyu anuai mikopo. Usisahau kwamba taasis hiyo pia ina jukumu la kuwapa mikopo wale wanafunzi wanaosomea ugaibuni. Kinaya ni kwamba bado hawajaongezewa  fedha kutoka hazina kuu ya kitaifa. Ndio maana tutaendelea kuona migomo ya wanafunzi wa vyuo wakilalamikia ukosefu wa pesa.

Fauka ya hayo, mgaala muue na haki mpe. Si wanafunzi wote ni watovu wa nidhamu. Wapo wenye maadili. Ukiwaangalia vizuri unaweza sema wana malezi ya pende mbili. Hao hufanya kile walinachostahili kufanya na hao ndio hutia for a katika Nyanja mbalimbali ya kimasomo na hata spoti. Na hao ndiyo kila mtu na hata selikali inajivunia.
 Ninapokamilisha ni vizuri kuuliza swali? Je ni nani anayestahili kulaumiwa ka kupungua nidhamu  katika vyuo vyetu?
Mwandishi ni Frankline Momanyi, Mwanafunzi  Chuo Kikkuu cha Chuka.

No comments:

Post a Comment