Kuwa mwanafunzi ni jambo nzuri sana haswa kwa taifa lolote
lile kwani linakuwa na matumaini ya kuwa na nguvu kazi ya kutosha kujenga
uchumi wa taifa. Ndio maana kila mja sasa yuko mbioni ili angalau kuongeza
kitembo chake cha elimu ili kujinyakulia nafasi katika enzi hii ya utandawazi,
baada ya wao kubaini ukweli wa msemo usemao ushikwapo shikamana.
Hii inasababishwa na wale wanaosema elimu ni ni mwanga, nami
nakubaliana nao mia fil mia. Lakini naomba kuangazia hali ya kuwa mwanafunzi wa
chuo kikuu hapa nchini Kenya. Ni jambo nzuri sana kwa kuwa lina haiba yake. Heshima
unaporudi kijijini na hata mitaani. Licha ya heshima kuna pia ile kasumba
kwamba wanafunzi wa chuo kikuu wana hela kwani wanapewa na selikali. Kinaya.
Nikirejelea maisha ya chuoni, wanafunzi wengi wanasumbuka sana
ili kusukuma maisha yao chuoni. ikiwa mwanafunzi anatoka katika familia ya
ukabwela, ndiko kuna balaa. Naelewa si mapenzi ya mtu kuzaliwa katika katika
familia maskini. Lakini wengine wao wanafunzi wanaotoka lkatika familia maskini,
hupatana na maisha ya wenzao ambao wanatoka katika familia tajiri ama kwa jina
ingine wenye cheo na mbao si walala hoi.
Unawapata wanaanza hali ya kujiweka katika maisha ya juu
ambayo kuyamudu ni lazima ujifunge kibwebwe. Ndo sababu kuu kupata wengine
wanapania kujiunga na makundi ya ulanguzi wa mihadarati. Siku hizi wanafunzi
wengi wa jinsia ya kike naya kiume wote wamekimbila usherati. Na kwa sababu ya
utandawazi, wanaweza kwepa kwenda kwenye vijia lakini wanatumia mitandao ya
jamii kutafuta shugamummy ama shuga
dadi. Hawa ni waume na wake
wenye wamea ama kuolewa katika jamii. Wanatafuta hawa wadogo wanaohitaji hela
na wao wamalize mahanjam……
Ni vizuri ujue kwamba si wote wanaofanya hivyo kwani kuna
wale wanaoshikilia kindakindaki maadili ya jamii. Hongera! Wao hujituma kwa
kazi yeyote ile nzuri ili kuunga shilingi moja mbili kwani wanaelewa kwamba
haba na haba hujaza kibaba. Wengine wamekuwa machinga. Wao huchuuza vitu hapa
na pale ili kutengeneza shilingi.
Najua unajiuliza, mbona wafanye haya yote? Naamini wanafanya
haya kwa sababu mahitaji ni mengi na hawana pesa. Ndio maana ubunifu wa kila
aina unahitajika ili kuwawezesha kujikimu kimaisha. Nimeona wengine wakiekeza hela zao
kidogo wanazopata kutoka kwa ruzuku ya
selikali. Ni vizuri ufaham kwamba kiwango cha ruzuku hiyo kimepungua kwa
kiwango kikubwa. Ndio maana kwa sasa wale wanaopahatika kupata wanapewa
shilingi 37,000 badala ya kiwango cha juu cha 60,000. Hili ni jambo la kutamausha sana lakini kutoka kwa tume hiyo
inayopeana ruzuku (HELB) Niliweza
kufunga safari mpaka huko ili nijue shida iko wapi. Nilielezwa kwamba hawana
hela za kutosha kwa kila mtu kupata kiwango cha juu. Ni heri wapeane
kidogokidogo ili wengi wapate.
Wakati mwingi baadhi ya wanafunzi hao hawatambui haya. Ni majuzi
tu, tuliona wanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi wakiadamana barabarani wakitaka
pesa. Kulingana nami, viongozi wa wanafunzi ndio hutaka tu maandamano hayo
kutokea katika taifa letu. Ninaijiuliza tu, Iwapo HELB haina pesa, watatoa wapi
kuwapa mkigoma na kuleta hasara yote? Na ilhali hata selikali yenyewe haina
pesa inaendelea kukimu mahitaji ya kaunti, ambazo mpaka sasa zinadai kupewa
hela zaidi kwa nyimbo zao za pesa mashinani!
Nikichukulia mfano, viongozi wa wanafunzi katika Chuo cha
Chuka, mimi nikiwa mmoja wao, sisi tunaelewa shida iko wapi na tunawaita
wanafunzi wetu tunawaeleza. Ikibidi kuleta afisa kutoka HELB aje afafanue hayo,
tunawaita na wao wako radhi kuitikia wito wetu. Kwa sababu tunaamini katika
Nguvu ya majadiliano. Sitasema kwamba hapa chuoni mwetu hamna shida. La hasha! Zipo
tena kibao lakini sisi tunazungumza kwenye meza na hili ni jambo nawaomba
wanafunzi wote kuiga.
Nikirejerea mada ya ukosefu wa hela, tunaona wanafunzi wengi
huwa wanakosa hata uwezo wa kulipa karo. Ndio maana sisi kama viongozi wa
wanafunzi Chuka, kuanzisha mpango wa kuwapa wanafunzi wetu ruzuku na wanakuja
kulipa baada ya wao kukamilisha masomo yao. Mipango ya kukamilisha hazina hiyo
imefika kileleni. Hivi karibuni, hazina hiyo itazinduliwa rasmi. Na naamini
itakuwa na uwezo wa kusaidia wengi kulipa karo.
Na wito wangu kwa wanafunzi wote wa chuo kikuu, nyinyi ndio
kioo cha jamii. Nyinyi ndio mko katika kilele ya maisha kimasomo. Nawaomba msimame
kidete kipigania maadili ya jamii na musiwe ala za kuyavunja. Nidhamu ni chombo
imara na hata ukikumbwa na shia gani hata ikiwa ya pesa, jikaze na milango ya
kheri itafunguka siku moja. Na muelewe kwamba Rabuka si athmani.
No comments:
Post a Comment