Thursday 30 October 2014

Wazazi wapata afueni


Wanafunzi wa shule ya uoili wakiwa kwenye mahabara.

Mapendekezo yaliyotolewa na jopo la kutathmini karo za shule za upili ni mwafaka iwapo yataidhinishwa. Mapendekezo hayo ya kupunguza karo kwa wanafunzi wa shule za upili za umma yanafaa na ni afueni kwa wazazi ambao kidogo wamekuwa wakitwika mzigo mkubwa sana wa kulipa kitita kikubwa cha fedha kila mwaka.

Tume hiyo inayoongozwa na aliyekuwa wazili wa elimu Dkt Kilemi Mwiria ambaye sasa ni mshauri wa rais kuhusu maswala ya elimu iliwasilishe ripoti yenye mapendekezo hayo kwa rais ambaye aliyapokea kwa mwelekeo chanya na kusema kuwa kila motto anapaswa kupata elimu ya kimsingi. Aidha rais aliongeza kusema kuwa serikali kuu itashirikiana na idara nyingine pamoja na washikadau husika kuhakikisha kuwa hili litatimia.

Hatua hii itahakikisha kuwa visa vya wanafunzi kuacha shule kwa ajili ya ukosefu wa karo imezimwa hivyo kwa wanafunzi ambao huzembea katika masomo yao na kuacha shule hawatawa na sababu ya kuacha hivyo basi waweza wakachukuliwa hatua za kisheria. Hii pia itatoa nafasi sawa kwa kila mwanafunzi kupata elimu. Ni matumaini ya kila mzazi kuwa Rais ataidhinisha mapendekezo hayo baada ya mashauriano na washikadau wote katika sekta ya elimu.

 Mwandishi ni Mburu Samwel
(Chuo Kikuu cha Chuka.)

No comments:

Post a Comment