Thursday 16 October 2014

Hamas yaitaka UN iwajibike kuhusiana na Gaza



Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imetoa wito kwa Ban Ki -moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa awajibike kuhusiana na wananchi wa eneo linalozingirwa la Gaza, ambao wamekuwa wakitaabika kutokana na vita vya kichokozi vya hivi karibuni vya utawala wa Kizayuni. Sami Abu Zuhri msemaji wa Hamas amesema kuwa, Ban Ki Moon ameshiriki katika kuficha mauaji yaliyofanywa na Israel huko Rafah na kuongeza kuwa, anapaswa kuchukua jukumu kuhusiana na waathirika wa mashambulio hayo ya Israel na kuhisi mateso yao.
Watu 68 waliuawa na wengine zaidi ya 350 kujeruhiwa katika shambulio la askari wa Israel huko kusini mwa Ukanda wa Gaza katika mji wa Rafah tarehe Mosi Agosti. Jana Ban Ki-moon aliutembelea Ukanda wa Ghaza kwa mara ya kwanza tangu baada ya mashambulizi ya kinyama ya Israel dhidi ya raia wa eneo hilo. Ban ametaka ufanyike uchunguzi kuhusu kubomolewa shule huko Ukanda wa Ghaza katika mashambulizi yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kwa hisani ya IRIB World service.

No comments:

Post a Comment