Thursday 16 October 2014

Kiongozi wa MRC Atiwa nguvuni



Polisi  jana walimtia nguvuni kiongozi wa kundi linalotaka kujitenga eneo la Mombasa la Mombasa Republican Council (MRC) na wenzake kadhaa.
Omar Mwamnuadzi alitiwa nguvuni nyumbani kwake Kombani, Kaunti ya Kwale na baadaye alishtakiwa na kuwekwa rumande kwa siku saba kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Maafisa wa polisi waliovamia na kumkata mwenyekiti huyo wa MRC walitoka vikosi tofauti vya usalama nchini Kenya.
Watuhumiwa hao wa kundi la MRC wanakabiliwa na tuhuma kadhaa ikiwa ni pamoja na kufanya mkutano usio halali kinyume cha sheria.
Kundi la Mombasa Republican Council (MRC) linalotaka kujitenga eneo la Mombasa linalaumiwa na serikali kwa kuhusika na mashambulizi yaliyotokea katika eneo la pwani la Lamu katika miezi ya Juni na Julai mwaka huu yaliyosababisha vifo vya watu wengi.
Omar Mwamnuadzi 

No comments:

Post a Comment