Prof. Mazrui |
Kifo chake Prof. Mazrui si pigo tu
kwa Kenya bali ni kwa ulimwengu mzima. Alikuwa mmoja kati ya watu ambao
kuchezea kwenye kiwango chake ilikuwa vigumu. Kwa kweli Profesa Mazrui alikuwa vitu
vingi vilivyowekwa ndani ya mtu mmoja. Hakuwa tu msomi mtajika balialikuwa
shupavu wa kutetea haki za kibinadamu mwandishi aliyekamilika na pia
mchanganuzi wa maswala ya kisiasa.
Wakati ambapo wenzake walieneza
chuki za kikabila na tofauti za kidini yeye hakutawaliwa na mambo madogo kama
hayo. Yeye alishughulika na maswala ya kuelimisha ulimwengu kwa kusimama kidete
kutetea haki za wanyonge na waliotelekezwa mahali popote walipokuwa ulimwenguni.
Wakati ambapo wataalamu wengi waliogopa kukashifu uongozi wa kiimla yeye alisimama
wakati mmoja na kuingilia uongozi wa KANU na hili likasababisha yeye kunyimwa
kazi ya uhadhiri katika chuo kikuu cha Nairobi. Mageuzi mengi Kenya yalifaidi
kutokana kwa mchango wake adhimu.
Yeye alitupilia mbali dhana ambayo
ilikuwepo kwamba dini ya kiislamu ilikuwa ya vita tu. Hata baada ya mataifa ya
magharibi waliobuni uvumi kuhusu uislamu yeye hakusikia hata bali alishikilia msimamo
wake kwamba dini hiyo si ya kivita wala zogo la kila wakati. Kwenye maswala ya
kiakademia alichangia pakubwa katika taaluma ya usomi kupitia kazi zake aula.
Ni aibu kubwa katika karne hii kuona wasomi wengi wakitawaliwa na ubarakala na
ukabila jambo ambalo ni tisho kwa utaifa. Swali langu ni je mbona tuwe na
wasomi wengi ambao watawa wasumbufu kwa ajili ya chuki za kikabila? Kila wakati
usomapo makala unaweza ukatathmini mwandishi ametoka kwenye kabila lipi.
Hakuchoka kuandika maswala ambayo
ylisumbua bara la Afrika na watu wake. Wakenya wanaweza kufuata na kumheshimu
profesa Mazrui kwa kuzingatia na kufuata katiba ilivyo kwa kikamilifu. Roho
yake na iwatie motisha wengi wanaopania kuwa wasomi halisi wasiojikita katika
maswala ya ukabila, ubarakala na ubinafsi. Lala salama mtetezi wa haki za
kinadamu na msomi mtajika.
Mwandishi: MBURU SAMWEL.
No comments:
Post a Comment