JANGA KUBWA VYUONI
Wanafunzi wengi hupata furaha wanapopata fursa ya kujiunga
na chuo kikuu. Kwa mfano, nilipopata
barua yangu mwaka wa pili baada ya kuhitimu masomo ya kidato cha nne. Ilikuwa
furaha, shangwe, na nderemo kijijini mwetu kwa kuwa mwana wao alikuwa anajiunga
na chuo kikuu. Chuoni ni mahali ambapo mja akiingia akitoka atatoka akiwa mtu
wa thamani sana katika taifa lake. Ndo maana wote wanafuzu vyuoni huwa nguvu kazi ya taifa na wanatumuwa kuendeleza
uchumi wa dola. Lakini sasa, hiyo sifa imeanza kufifia na kudidimia. Kwa nini?
Kitambo kidogo,
wanafunzi waliofuzu kwenda chuo kikuu walikuwa wanakaa nje ya chuo kikuu kwa
mwaka mmoja na nusu ivi kabla ya kuingia chuoni. Lakini kutoka mwaka wa 2011, wakati Naibu wa
Rais, Bw. William Ruto alipokuwa Waziri
wa Elimu ya Juu, wanafunzi wamekuwa wakijiunga na vyuo moia kwa moja.
Jambo nzuri lakini kulingana na wakati huu, naona yapo maafa mengi yanakumba vyuo vikuu. Hawa
wanafunzi wanapata shida ya kudhibiti
mhemko na kutoamini kwamba apo vyuoni. Mahali ampapo pana uhuru wasio kadiria.
Uhuru mkubwa kiasi kwamba hamna sare za kuvalia, kila mmoja ana hiari ya
kuvalia gwanda analoliona lamfaa. Ndiposa sasa tunavyo zungumza, ukipitapita
vibarabara vya chuo chochote kile mfano ukiwa chuo cha Chuka, utatamaushwa na
mavazi utakayo yaona. Juzi mzazi mmoja alizirai alipomwona mwanaye amevalia
jinsi hakuwa ametarajia kawe.
Shida nyingine ni ulevi wa pombe na mihadarati. Kwa miaka
nimekwa chuoni mwaka wanne sasa, mwaka huu mambo yamekuwa makali kuliko miaka
yaote. Wanafunzi haswa wa kike wanabugia mvinyo hadharani bila kujali yeyote
wala kuogopa sheria kali za chuo. Zinawafanya mpaka kupigana kisha kuvunja
sheria za chuo. Linalonishangaza ni kwamba hawana habari kwambahapa hakuna
kutumwa mzazi nymbani! Ole wao kwa sababu wengi wako mbioni kuonana na jopo la kushughulika
nidhamu.
Nimeshuhudia mimi wanafunzi wakipatatna asubuhi mchana
wameoana na jioni wanafukuzana kisha kesi naletewa mimi. Ngono kiholelaholela,
na kutofwatilia ule mpangilio uliowekwa ili kuendesha maisha chuoni. Hili limekuwa
likiwapa tumbo joto viongozi wa wanafunzi vyuoni nikiwa mmoja wao. Haswa idara
yangu ikiwa ni ya kushughulikia maslahi ya wanafunzi chuoni.
Badala ya kusoma, wapo mtandaoni wakitumia mtandao
kuwasiliana, katika mitandao ya kijamii. Maadam tovuti za ngono zimefungwa,
hawangebanduka mle. Mtihani ukifika,
baadhi yao wanandika mpaka ukuta almradi wapiti kwa kuwa wakianguka hamna
jingine ila kwenda nyumbani. Ndo sababu ya kufanya lolote kuokoa maisha yake
chuoni.
Nimeona uongozi umejaribu kuweka mikakati ya kukabiliana na
haya lakini bado maji yamezidi unga. Ninawaona washauri na saha wakiwa mbioni
lakini mbio zao ni za sakafuni ambazo mpaka sasa zinaishia ukingoni. Makundi ya
madhehebu mbalimbli mbalimbali chuoni yakijaribu kuleta msaada. Bado sijaoni
dalili ya matumaini.
Kulingana nami, kuwa katika nafasi ya kurudisha hadhi ya
chuo kikuu, lazima warudishe ule mfumo wa kitambo. Kuokoa malemgo ya chuo kikuu
kisimama imara, sharti serikali irudishe ule mfumo wa kitambo ili hawa
wanafunzi wapate kuona maisha kudogo kabla ya kujiunga na chuo kwa sababu hilo
litafawafanya kubadili msimamo wao kuhusu maisha na kutia bidii. Na pia kukomaa
kidogo.
Pili nimeletewa kesi nyingi sana za wanafunzi ambao hawana
pesa za kuwafanya wawe chuoni. Nikiangalia wale wengi wanakuja katika hali ya
uchochole kwa sababu ya msingi wa familia labda. Lakini ukiangazia vizuri, huyu
mwanafunzi angekubaliwa kukaa nje kwa miaka miwili kama ilivyokuwa zamani,
angetengeneza hela kidogo za kumsaidia kusukuma maisha. Akifika chuoni, ni
kuamsha balaa na belua. Hata kukidhi mahitaji yake ni shida. Karo nayo ni mlima
unaowapa kiwewe kuukwea.
Kwa sasa inabidi
ukumbuke kwamba ile taasisi ya kupoeana mikopo kwa wanafunzi wa vyuo
(HELB) pia haina hela za kutosha kukidhi
mahitaji ya wanafunzi wengi wanaongezeka kila kukicha. Pia taasisi hiyo haina lingine
ila kutekeleza amri ya selikali ya kusema iwape wanavunzi wa vyu anuai mikopo. Usisahau
kwamba taasis hiyo pia ina jukumu la kuwapa mikopo wale wanafunzi wanaosomea
ugaibuni. Kinaya ni kwamba bado hawajaongezewa
fedha kutoka hazina kuu ya kitaifa. Ndio maana tutaendelea kuona migomo
ya wanafunzi wa vyuo wakilalamikia ukosefu wa pesa.
Fauka ya hayo, mgaala muue na haki mpe. Si wanafunzi wote ni
watovu wa nidhamu. Wapo wenye maadili. Ukiwaangalia vizuri unaweza sema wana
malezi ya pende mbili. Hao hufanya kile walinachostahili kufanya na hao ndio
hutia for a katika Nyanja mbalimbali ya kimasomo na hata spoti. Na hao ndiyo
kila mtu na hata selikali inajivunia.
Ninapokamilisha ni vizuri kuuliza swali? Je ni nani
anayestahili kulaumiwa ka kupungua nidhamu
katika vyuo vyetu?
No comments:
Post a Comment