Ni jambo la kutamausha kuona yale yanayowasibu wachuuzi
katika jiji la Nairobi. Ni dhuluma kwa kaka na dada zetu wakenya wanaojitahidi
kutafuta cha kutia mdomoni. Lakini sasa kuwa machinga limekuwa ni jambo ambalo
si la kuvutia Miongoni mwa wakaazi wa jiji la Nairobi. Mbona kusumbuliwa na
kufanyiwa madhila yote na wao wanajitafutia cha halali? Kweli myonge hana haki.
Inauma kuona zile hela umewekeza katika katika biashara yako
kama mtaji ikigeuzwa jivu na askari ambao wanafaa kukutetea wewe kama mlipa ushuru.
Askari wa kaunti wamekuwa wakiwadhulum machinga wa jiji la Nairobi haswa pale
ngara, na eneo la globe cinema.
Wanawake wakishikwa wanaweke wakikamatwa, ni kunyanganywa hela zao, wengine
wanavuliwa nguo zao na hata kubakwa ndani ya magari yao. Na waume nao
wakishikwa, wananyanganywa hela zao na kuchomwa visu licha ya kupokea kichapo
cha mbwa mskitini.
Swali langu ni kwamba mbona wawe wanawadhulum na kuwapiga
vile? Najua utasema kwamba kuna sababu. Kulingana na vile nimeona wakifanya,
askari wa jiji wanawafukuza kutoka eneo la fig
tree kwa madai kwamba wanataka kujenga bustani, mara stendi ya basi, mpaka
sasa hawajapewa mahali pa kwenda. Mimi naelewa ukifukuza mtu atoke mahali
anafanyia biashara yake, basi mpe mahali mbadala ya kufanyia kazi yake.
Wachuuzi wa soko wakitoroka askari
wa kaunti ya Nairobi katika eneo la Globe Cinema.
|
Kuchukuwa mali yake na kugawana yanayobaki mnachoma si jambo
la halali. Na jambo la kukeketa maini ni kwamba askari wa taifa huwa wako pale
wanaangalia tu. Mchuuzi akiumizwa aende kupiga ripoti mara nyingi wanasema “ni
bahati hawakukuuwa” na hawa askari wamekula kiapo cha utumishi kwa wote! Kinaya
Na kulingana na ripoti ya viongozi wa kaunti ya Nairobi, wao
wamesema hawajui kama swala hilo lipo. Lakini itakuwaje wakenya walipa ushuru
kuumizwa kiasi kile na mseme hamjui? Swali linguine naulizwa kwani wale nanaotetea
haki za binadam, wako wapi kutetea hawa machinga? Ama jambo linakuwa la kukiuka
hali za kibinadam wakati bwenyeye amekosewa na wakati mtu wa kawaida amekosewa
sio jambo la haki za kibinadamu?
Ni vizuri kuonyesha kwamba, ndio wachuuzi hao huwa na hulka mbaya, hulka
ya kutumia nguvu. Hulka ya kuwafanya askari wa jiji watumie silaha butu ili kujaribu kuleta nidhamu lakini mbona
kujinyakulia haki mkononi? Tangu lini mtu akatiwa nidhamu kwa kuchomwa kisu? Mimi
naelewa ipo sababu ya haya kutokea. Baadhi ya askari wengi wa kaunti ya Nairobi
huwa wanataka kitu kidogo na iwapo mchuuzi hayupo radhi kumpa basi wananyakua
bidhaa zake na kuchukuwa ama wanachoma mchuuzi akiangalia. Na jambo hili
linawafanya wawe na mawazo hasi haswa yanayo wafanya wawe wakivunja sheria
zilizoko kwa machungu ya kudhulumiwa. Ikiwa mtu amekosea, mshike na ushahidi
kisha mpeleke mahakamani ahukumiwe kulingana na mujibu wa sheria.
Mimi naomba selikali kuu iingilie swala hili kuwasaidia
wakenya wanaojitetea kutafuta riziki. Pia selikali ya kaunti kuketi chini na
viongozi wa wachuuzi ili kutafuta suluhu kwa jambo hili. Pili lile kundi la
kutetea haki za kibidamu liingilie kati. Lakini ni muhimu kuzingatia maridhiano
baina ya pande zote mbili ndilo jibu tu la tatizo hili.
No comments:
Post a Comment