Thursday 9 October 2014

MTI MREFU ZAIDI NCHINI

       
MUTUNGURUNI. Hilo ni jina la mti unaoaminika kuwa mrefu sana katika Kenya na Africa Mashariki,  kaunti ya Tharaka Nithi, eneo wakilishi bunge la Chuka Igamba-Ng`ombe. Eneo hili liko takriban kilomita tano tu, kutoka kwa lango kuu la Chuo Kikuu cha Chuka.
 
Mti huu unapatikana katika eneo la mashariki na inaaminika kuwa mti huo umekuwa duniani zaidi ya miaka mia nne, walivyosema wakaaji wa sehem hii. Inakisiwa kwamba mti huu u zaidi ya mita themanini na tano. Na umekuwa mojawapo ya kivutio cha watalii wanaozuru kaunti hii ya Tharaka Nithi.
 
Kulingana na mjuzi wetu, viongozi wa eneo hili wapo radhi kutwaa raslimali hii na kuhakikisha kwamba ipo katika hali ya kukuzwa na kuleta fedha katika kaunti.
 
Hizi ni picha za mti huo - Mutunguruni

 
 
 
 
 

 



Picha hii inaonyesha shimo kubwa pana lenye urefu wa futi zaidi ya sita na ambalo liko katikati ya mti huo.

No comments:

Post a Comment